tuwasiliane

Sunday, February 12, 2012

12 FEB.SIMBAA YAFANYA KWELI

Simba SC JANA,imewapa somo Azam FC katika uwanja wa Taifa baada ya kuwachapa goli 2-0 na kutandaza Soka safi katika kipindi cha kwanza na kuwaacha Azam wakikosa mbinu ya kupenya ngome ya Simba katika kipindi cha pili.

Simba waliteremka uwanja kwa dhumuni ya kuwafurahisha na kurudisha imani kwa mashabiki wao, wakati Azam FC wakiwa na dhamira ya kuongoza ligi kwa masaa kwa kuwafunga Azam.

Kati ya dakika ya 15 na 30 walimiliki mpira kwa Zamu huku John Boko akipoteza nafasi, huku akionekana yuko nnje ya mchezo.

Ilikuwa ni dakika ya 31, Emanuel Okwi akiwanyanyua mashabiki wa Simba kwa shuti hafifu lililopigwa katikati ya msitu wa mabeki wa Azam na kumshindwa kipa Mwadini aliyecheza chini ya kiwango.

Baada ya goli hilo lililodumu mpaka mapumziko Azam FC walianza kuonekana kupoteza mwelekeo pale wanapokaribia lango la Simba SC.

Kipindi cha pili kilitawaliwa zaidi na Azam huku kukishuhudia Saidi Moradi na Kago wakigongana na kupelekea kushindwa kumalizia pambano.

Simba walitumia mashambulizi ya kushtukiza katika kipindi cha pili wakati Azam wakipoteza nafasi kadhaa zakujiandikia bao.

Ilikuwa ni Dakika ya 65 ambapo Emanuel Okwi alipokea mpira mrefu uliomshinda kuuzuia mlinzi wa Azam, hivyo Okwi akamchambua vilivyo Mwadini Ally na kufunga goli la pili.

Kwa matokeo hayo Azam FC wamepoteza mchezo wa kwanza kwa Simba chini ya kocha Stewart Hall na Simba kukwea mpaka kileleni mwaligi.


Wakati huo huo Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani Coastal Union wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachapa goli 1-0 African Lyon.

Goli pekee la ushindi kwa wagosi wa kwaya lilifungwa na Ahmed Shiboli katika dakika ya 32.

Katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, Nsa Job akifunga katika kila kipindi aliwapa ushindi wa goli 2-1 Villa Squad dhidi ya Polisi Dodoma.

Katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza Toto Africa wameshindwa kutamba baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Moro united.

Na katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kulishuhudia tumaini jipya la Arusha JKT Oljoro wakipoteza mchezo wa tatu mfululizo, kufuatia goli la kiungo wa JKT Ruvu kutokea Simba Mohammed Banka.

Goli hilo la Banka limeitoa kifua mbele JKT Ruvu kwa kuichalaza Oljoro goli 1-0.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (17) 37
2. Yanga (16) 34
3. Azam FC (17) 32
4. JKT Oljoro (17) 26
5. JKT Ruvu (17) 23
6. Mtibwa Sugar (16) 22
7. Kagera Sugar (16) 20
8. Coastal Union (17) 20
9. Ruvu Shooting (16) 18
10. African Lyon (16) 17
11. Villa Squad (17) 16
12. Moro United (17) 16
13. Toto Africa (16) 14
14. Polisi Dodoma (17) 13

No comments:

Post a Comment