tuwasiliane

Friday, February 3, 2012

03 FEB.BREAKING NEWS; Mtibwa Sugar Yamsimamisha Mecky Mexime.


Taarifa kutoka huko mkoani Morogoro zinasema kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar FC. Meck Mexime amesimamishwa baada ya wachezaji kumkataa
taarifa inasema wachezaji wa Mtibwa Sugar walikua na mgomo baridi uliosababisha timu hiyo kupoteza michezo miwili mfululizo kwenye uwanja wake wa manungu dhidi ya JKT Oljoro na Coastal Union .
baada ya uongozi wa juu wa Kiwanda kukaa na wachezaji hatimae wachezaji hao wakasema hawamtaki ndani ya timu. Na ndipo utawala wa kiwanda ukaamua kumsimamisha kazi pamoja na wachezaji wengine wawili.

SOURCE SHAFFIH DAUDA AND TBC1

No comments:

Post a Comment