tuwasiliane

Thursday, February 2, 2012

02 FEB.Cheka: Wembe utakao tumika ni ule ule


Kwani Pambano hilo ni la kuwania Ubingwa wa Afrika Mashariki wa IBF, Uzani wa Super Middle linatakalotambuliwa na Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) litafanyika ndani ya Ukumbi wa PTA, Sabasaba uliopo hapa Jijini.

Pambano hilo linawakutanisha Bondia Mada Maugo 'Mbunge wa Rorya' wa hapa Jijini, amepata nafasi ya kurudiana na mbabe wa masumbwi uzani wa kati nchini, Francis Cheka ‘SMG’ wa Morogoro na litawika hapo Aprili 28 mwaka huu.

Naye Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraji, tayari mabondia hao wamekubali kupanda ulingoni kumaliza ubishi wa nani mbabe wa ukweli baina yao kwani Mada aliyepigwa kwa pointi walipokutana kwenye ukumbi huo mwaka jana amekuwa akipinga matokeo hayo.

Alisema maandalizi ya awali ya pambano hilo yamekamilika na kwamba leo mabondia hao watazungumza na waandishi wa habari.

Alisema kwamba wameamua kuanza maandalizi ya pambano hilo mapema ili kuepusha ubabaishaji, ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya waandaji na kwamba watazingatia sana suala la ulinzi na usalama kwa mashabiki.

Kwa upande wa Maugo alisema anafurahi kupata nafasi hiyo muhimu ya kurudiana na Cheka na kwamba mbali ya kuthibitisha ubabe lakini pia safari hii atafurahia kuvikwa mkanda wa ubingwa.

Cheka alisema wembe aliotumia kumuadhibu Maugo walipokutana ataugeza upande wa pili huku akiwa ameuongezea makali ili aweze kutwaa ubingwa huo.

No comments:

Post a Comment