tuwasiliane

Friday, December 16, 2011

16 DEC.DARAJA LA KIGAMBONI HILOOOOOOOOOOOOO


Baada ya miaka nenda rudi ya Longo longo kibao, hatimae
kampuni tano za Ujenzi zimeingia kwenye ushindani kuwania zabuni ya ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa zabuni ya ujenzi wa daraja hilo, Bw. Ludovick Mrosso, makampuni hayo yameingia kwenye droo ya mwisho itakayotoa mshindi hivi karibuni.

Alisema awali kampuni saba za ujenzi zilijitokeza kuomba zabuni hiyo ya kujenga daraja la Kigamboni na kwamba baada ya kutakiwa kuthibitisha uwezo wao kifedha mbili zilichapa lapa (zilijitoa) na tano kuthibitisha kuwa na vigezo vilivyotakiwa.

Alizitaja kampuni zilizoonyesha jeuri ya kuwa na mkwanja wa kuanza ujenzi huo kuwa ni Long Jian Road and Bridge Limited ya kichina, Schuan Road and Bridge Group Lilimited pamoja na China Communication Constructon Limited.

Kampuni nyingine ni China Railway Construction Engineer Group na China Major Bridge Engineer Limited na Chong Qung.

Imeelezwa kuwa baada ya kampuni hizo kuthibitisha kuwa na uwezo wa akiba ya fedha za kuanza ujenzi, Kamati itakutana na kupitisha jina la kampuni itakayoanza ujenzi wa daraja hilo.

No comments:

Post a Comment