KAMATI ya Ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),itahakiki vyeti vya Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic ili kuona kama anastahili kuifundisha timu hiyo duru la pili wa Ligi Kuu Bara.Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema jana kuwa Kamati imepokea vyeti hivyo jana na kitakachofuata ni kuvihakiki ukweli wake.
Angetile alisema utaratibu unataka kocha yeyote anayefundisha Ligi Daraja la kwanza na Ligi Kuu kuwasilisha vyeti vyake ili kuthibitisha kama anakidhi viwango husika.Alifafanuwa kuwa huu ni utaratibu ambao upo siku zote hata kwa kocha Moses Basena ambaye hakuleta vyeti vyake na ilikuwa asiinoe Simba kwenye mzunguko wa pili.
"Huu ni utaratibu wa kawaida ila tatizo ni kwamba, viongozi wa klabu huleta makocha kinyemela," alisema Angetile na kutolea mfano kocha wa Simba, Moses Basena ambaye alishindwa kuleta vyeti vyake.
"TFF isingekubali Basena aendelee kuifundisha Simba mzunguko wa pili bila kuleta vyeti halisi vya taaluma yake na kuvithibisha," alisema Osiah.Osiah alisema endapo Kamati ya Ufundi itaona mapungufu vyeti vya Milovan, itavirudisha ili vifanyiwe marekebisho ndipo aruhusiwe.
"Haya mapungufu yameonekana kama utaratibu wa kawaida kwa klabu nyingi, lakini sasa tunataka kuona hayatokei tena," alisema zaidi Osiah.
No comments:
Post a Comment