
Madenti wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wamegoma kuingia Class kwa muda usiojulikana kushinikiza uongozi wa chuo hicho kurudisha madenti waliosimamishwa masomo.
Wakizungumza huku wakiwa na jazba jana baadhi ya madenti hao walisema mgomo huo utaendelea hadi wanafunzi waliosimamishwa masomo warudishwe.
Walisema Novemba 11 wanafunzi waligoma chuoni hapo kushinikiza wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatiwe mikopo lakini baadhi ya wanafunzi walikamatwa na askari na kupelekwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.
Baada ya madenti hao kukamatwa na kufikishwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu walifunguliwa kesi ya kufanya mikusanyiko isikuwa halali.
Alisema kuwa baada ya kufunguliwa mashtaka hayo walirudishwa rumande hadi hapo uongozi wa chuo ulipoenda kuwatolea dhamana.
Waliporudi chuoni wanafunzi 35 walipewa barua za kukaa nyumbani hadi hapo kesi itakapoisha ndipo warudi chuoni.
Madenti wengine 15 wamepewa barua za onyo na wengine 8 wamesimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa hadi mwakani.
Bw. Mabrika Mawazo ambaye ni denti wa mwaka wa pili alisema kuwa, kama wanafunzi hao wamesimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa wangesimamishwa wanafunzi wote kwani maandamano yalifanywa na wanafunzo wote.
Pia alisema kuwa maamuzi yaliyotolewa na chuo hicho kufukuza wanafunzi hao siyo ya haki bali wangeondolewa wanafunzi wote.
Alisema kuwa hata serikali ya wanafunzi (DARUSO)
imeungana na utawala kukandamiza wanafunzi hao.
Pia alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kutopewa madaraka ya kuchagua makamu Mkuu wa chuo ili kuondoa siasa vyuoni.
"Rais atakiwa kupewa madaraka ya kuchagua makamu Mkuu wa chuo anatakiwa kuteuliwa na maprofesa wenyewe ili aweze kuwa na nguvu ya kutoa maamuzi,"alisema Bw. Mawazo.
No comments:
Post a Comment