tuwasiliane

Sunday, December 11, 2011

11 DEC.SIMBA KUMFUNGIA BOBAN


UONGOZI wa Simba utamchukulia hatua za kinidhamu kiungo wake Haruna Moshi 'Boban' kutokana na kitendo chake utovu wa nidhamu alichoonyesha katika michuano ya Chalenji.

Boban aliondoka kwenye benchi bila mawasiliano na viongozi wakati wa mechi dhidi ya Zimbabwe, ambayo Kili Stars ilifungwa 2-1. Kwa kitendo hicho, alitimuliwa kambini.

Akizungumza na jijini jana, Afisa habari wa Simba, Ezekieli Kamwaga alisema hawajapata ripoti ya utovu wa nidhamu toka Shirikisho la soka Tanzania, TFF, lakini watakapopata watatoa uamuzi.

"Nimeuliza TFF kama tayari wamepata ripoti ya Moshi, wamesema wanasubiri mpaka mwisho wa mashindano. Tukishaipata tutachukua hatua za kinidhamu ili iwe fundisho,"alisema Kamwaga.

Katika hatua nyingine, Kamwaga alisema programu rasmi ya Kocha Curkovic Milovan itaanza Jumatatu baada ya wachezaji wote kumaliza majukumu yao kwa ajili ya kujipanga na mbio za mzunguko wa lala salama wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Alisema tayari wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na watatumia wachezaji wote na wale wa timu ya vijana chini ya miaka 20.

No comments:

Post a Comment