tuwasiliane

Sunday, December 11, 2011

11 DEC .Yanga kuanza na Zamalek


MABINGWA wa soka Tanzania bara, Yanga wamepangiwa kuanza kampeni za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani dhidi ya Zamalek.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jana, Yanga wataanza nyumbani kati ya Februari 17, 18 na 19 kabla ya kurudiana kati ya Machi 2, 3 na 4.

Aidha, timu itakayoshinda mechi hiyo ya awali, itacheza na mshindi wa mechi kati ya Missile ya Gabon na Africa Sport ya Ivory Coast.

Mechi hizo zitachezwa kati ya Machi 23, 24 na 25 na marudiano itakuwa kati ya Aprili 6, 7 na 8.

Kwa upande wa Simba itakayoiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho itaanza kampeni zake ugenini Rwanda dhidi ya Kiyovu FC.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mshindi wa mechi hiyo atacheza na AS Setif ya Algeria.

Kwa upande wa wawakilishi wa Zanzibar, Mafunzo itaanza Ligi ya Mabingwa kwa kumenyana nyumbani na Muculmano de Maputo ya Msumbiji na ikifanikiwa kuvuka hatua hiyo itacheza na Dynamos ya Zimbabwe.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, timu ya Jamhuri itacheza na Hwange ya Zimbabwe na mshindi wa mechi hiyo atacheza na El Amal Otbara ya Sudan.

Katika michuano iliyopita, wawakilishi wote wa Tanzania Bara na Zanzibar hawakufanya vizuri
waliishia hatua ya awali na kuaga mapema.

No comments:

Post a Comment