tuwasiliane

Saturday, November 5, 2011

YANGA,TIMBE WAENDELEA KUVUTANA


PAMOJA na uongozi wa Yanga kudai kuwa wameshamalizana na kocha waliyevunja naye mkataba, Sam Timbe, mwenyewe amesema mpaka kufikia jana jioni hakuwa amelipwa hata shilingi.
Mbali na kutolipwa madai yake, pia alisema hafahamu hatima yake baada ya mkataba wake kusitishwa wiki moja iliyopita.

Akiongea na Mwananchi jana, Timbe alisema hafahamu hatima yake kwa vile mpaka sasa hajaelezwa lolote na uongozi wa Yanga.
"Sijalipwa hata shilingi na sijaelezwa ni lini watanilipa. Siwezi kuondoka Tanzania bila kulipwa madai yangu," alisema Timbe.

Timbe kocha raia wa Uganda aliyeipa ubingwa wa Bara na Kombe la Kagame alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Kostadin Papic.
Lakini jana hiyo hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa alipoulizwa kuhusu madai ya Timbe alitoa majibu tofauti.

"Kimsingi ni tumeshamalizana naye, na (kesho) leo anaweza kuondoka nchini," alisema Mwesigwa.
Lakini Timbe alipoulizwa juu ya safari yake ya leo, alisema kwa ufupi: "Sijui kama naondoka leo, ila kama ni kweli nitashukuru lakini ni lazima nilipwe changu," alisema.

Wakati huo huo, wachezaji wa Yanga jana walizawadiwa Sh50 milioni kama zawadi kufuatia kuifunga Simba bao 1-0 katika mechi ya kwanza msimu huu wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa wiki moja iliyopita jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya pili kwa wachezaji hao kutunzwa kutokana na kuifunga Simba, ambapo mara ya kwanza ilikuwa katikati ya wiki hii, ambapo walipewa Sh10 milioni kutoka kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Devis Mosha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa alisema fedha hizo ni kwa ajili ya wachezaji wote na Benchi la Ufundi.

Selestine alisema kuwa fedha hizo ni utekelezaji wa ahadi waliyoitoa kwa wachezaji endapo wangeifunga Simba.
Bosi huyo hakuweka wazi kiwango cha kila mchezaji, lakini alisema viwango vinatofautiana kulingana na mchango wa kila mchezaji ila hakuna aliyepata chini ya shilingi Sh1 milioni.

Aidha, kutoka mjini Dodoma timu ya Yanga imeendelea kuweka rekodi ya mapato kwenye Uwanja Jamhuri mjini hapa baada ya kuingiza sh28 milioni katika mchezo dhidi ya wenyeji Polisi Dodoma katikati ya wiki hi.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kufunga duru la kwanza, Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Kwa mujibu wa rekodi za uwanja huo, Yanga ndio timu pekee ambayo kila inapocheza mapato huwa makubwa.
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1977 Uwanja huo kuingiza mapato makubwa kiasi hicho.

Msimu uliopita Yanga ilipocheza na timu hiyo, zilipatikana sh20 milion

No comments:

Post a Comment