tuwasiliane

Saturday, November 5, 2011

06 november 2011 .Damaturu Nigeria yashambuliwa




kikundi cha kiislam cha bokoharamu kinadai kimefanya shambulio kaskazini mwa nigeria,kimedai kimeua watu zaid ya 65

Taarifa zinazohusianaAfrika, SiasaMsemaji wao alilielezea gazeti moja la Nigeria, kwamba mashambulio zaidi yatafwata.

Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu aliarifu kuwa karibu mauaji yote yalitokea katika mji wa Damaturu, ambako makao makuu ya polisi yalishambuliwa na mtu aliyejitolea mhanga.

Makanisa kadha piya yalishambuliwa kwa maguruneti.

Ghasia zilianza Ijumaa katika mji ulio jirani, wa Maiduguri, ambapo kambi ya jeshi ilishambuliwa na mtu aliyejitolea mhanga.

Wakuu wa Nigeria walionya kwamba kunaweza kutokea mashambulio kabla ya sikukuu ya Idd hapo kesho.

No comments:

Post a Comment