
'
MAMA mzazi wa mwanamuziki Rehema Chalamila 'Ray C' amesema ana imani kubwa kwamba ipo siku mwanaye huyo atafuata nyayo zake kwa kuokoka na kuachana na mambo ya dunia.
"Mimi nimeokoka na watoto wangu pia wameokoka, lakini amebaki Ray C ambaye hata hivyo kila siku nimekuwa nikimuomba Mungu naye amjalie aokoke ili aweze kumtumikia Mungu kikamilifu," Mama Chalamila alimwambia rafiki yake Ray C mjini Iringa wikiendi iliyopita na Mwanaspoti kuinasa kauli hiyo ingawa mama huyo hakupenda kuingia kiundani.
Habari zinasema kuwa mama huyo amekuwa akikabiliana na wakati mgumu licha ya nia yake ya kutaka kumbadili mwanaye ambaye ni mwanamuziki nguli wa kidunia.
Msanii huyo imeelezwa kuwa kwa sasa yupo nchini Marekani kikazi na makazi yake amehamishia jijini Nairobi, Kenya.
No comments:
Post a Comment