
MSANII wa muziki wa Bongo, Diamond, amesema kitendo cha kumvisha pete ya uchumba mlimbwende na muigizaji wa filamu za Bongo, Wema Sepetu, hajakifanya kwa makisio bali amekusudia na ameona anafaa kuwa mke wake.
Uamuzi huo aliuweka wazi katika siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam, akisema kuwa Wema ni mwanamke aliye na umuhimu mkubwa katika maisha yake.
"Nimekuwa na uhusiano na wadada wengine lakini huyu Wema nawahakikishia kuwa ni muhimu sana kwangu na pia anastahili kuwa mke wangu na ndiyo maana leo nimeamua kuweka hadharani mwanzo wa uhusiano huu," alisema Diamond.
Diamond anayetamba na wimbo wa Moyo Wangu pamoja na vibao vingine kama Mbagala na Kamwambie, akionekana mwenye furaha na akasisitiza kuwa ataharakisha kufunga ndoa na Wema.
No comments:
Post a Comment