Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, umekamilika kwa Wallece Karia kuibuka kidedea wa kiti cha Urais baada ya kupata kura 95 (asilimia 74.22) ambazo hazikuweza kufikiwa na wagombea wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Karia alikuwa Makamu wa Rais kwenye uongozi uliopita ambao ulikwa unaongozwa na Jamali Malinzi, aliye enguliwa kwenye uchaguzi huo kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za TFF, yeye na Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
Karia ameibuka mshindi katika nafasi ya Rais, baada ya kuwashinda wapinzani wake Ally Mayayi na Shija Richard ambao wote walipata kura tisa Iman Madega aliyepata kura nane, Fredrick Mwakalebela kura tatu na Emmanuel Kimbe aliyepata kura moja.
Katika nafasi ya Makamu wa Rais aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania FAT sasa TFF, Richard Wambura alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 85 ( asilimia 66.4) na kuwabwaga wapinzani wake Mulami Nghambi aliyepata kura 25,Mtemi Ramadhani kura 14 na Robart Selasela aliyeambulia kura mbili.
Baada ya kuapishwa Rais Mpya wa TFF, Karia alitoa hutuba fupi ambapo aliitaka Kamati yake kuchapa kazi kwa bidii ili kurudisha imani ya Watanzania katika mchezo huo ambao unaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini.
Karia alianza kwa kuwashukuru wajumbe kwa kuonyesha imani kubwa kwake hata kumchagua yeye kuwa kiongozi mkuu wa TFF, na kuahidi kuwatumikia kwa nguvu zake zote ili kufika kule ambako wamekusudia.
“Katika ilani yangu nina vitu 11, ambavyo vinaonekana vidogo, lakini siyo hivyo kama wanavyodani nitahakikisha navisimamia kwa umakini ili kurudisha mpira wa Tanzania kwenye levo inayotakiwa,”alisema Karia.
Kiongozi huyo alisema katika uongozi wake atajitahidi kutoa mafunzo mbalimbali ikiwemo na kwa waandishi wa Habari ili waweze kufanya kazi yao kwa umakini na wawee kusaidiana ili mambo yao yaweze kwenda sawa.
No comments:
Post a Comment