Shirikisho la soka nchini Morocco limetangaza kuwa linasema uwa litawasilisha ombi la kuandaa kombe la dunia 2026.
Fifa tayari imethibitiha kuwa ilipata ombi hilo la kuandaa mchuano huo kutoka taifa hilo la Afrika kufikia siku ya ijumaa.
Marekani, Canada na Mexico tayari zilikuwa zimetangaza mnamo mwezi Aprili kwamba zinataka kuandaa dimba hilo ka ushirikiano.
Kombe la dunia liliwakuandaliwa na Afrika Kusini 2010 na hii itakuwa mara ya tano kwa Morocco kuwasilisha ombi.
Shirikisho la soka barani Africa Caf iliunga mkono ombi hilo la Morocco mnamo mwezi Julai.
Jumla ya timu 48 badala ya 32 zitashiriki katika kinyanganyoro kilichopanuliwa na kuongezwa idadi ya timu 2026 baada ya mabadiliko kutangazwa mwaka huu.
Uamuzi kuhusu ni nani anayefaa kuandaa dimba hilo utafanywa 2020.
Sera ya Fifa ya kuandaa dimba hilo kwa zamu inamaamisha kwamba Afrika ni mojawapo ya mashirikisho ambayo yanaweza kuandaa fainali za 2026 kwa kuwa Ulaya itaanda mwaka 2018 kupitia Urusi na Asia ikiandaa 2022 kupitia Qatar.
No comments:
Post a Comment