Klabu ya Yanga inatarajia kukamilisha zoezi la usajili wake kwa kipindi hiki cha kiangazi siku ya Jumapili kwa kumsajili beki wa kati raia wa Nigeria Henry Tony Okho.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Yanga, Husseni Nyika amekiambia chanzo chetu kuwa, kabla ya siku hiyo pia wameshawasainisha wachezaji wawili hivi karibuni ambao ni, Matheo Anthony na Papii Kabamba T’shishimbi.
“Ni kweli Jumapili tutafunga usajili kwa kishindo kwa kumtangaza mmoja wa wachezaji wakubwa na hapo ndiyo itakuwa mwisho wetu kwa msimu huu hadi hapo dirisha dogo,” amesema Nyika.
Nyika amesema usajili wao msimu huu wameufanya kisayansi kwa kuzingatia mapungufu yaliyokuwepo kwenye kikosi chao hivyo imani yao kwamba hakutakuwa na kikwazo zaidi ya ubingwa kama walivyofanya misimu mitatu iliyopita.
Amesema kwa sasa kikosi chao kipo mkoani Morogoro, kikijiandaa na msimu mpya wa ligi hiyo abayo wamepania kufanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma.
Kikosi cha wachezaji waliopo kambini Morogoro ni Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, Nadir Haroub ‘Cannavaro’. Kevin Yondan, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Andrew Vincent ‘Dante’, Mwinyi Mngwali,Abdalla Haji ‘Ninja’.
Wengine ni Said Juma ‘Makapu’, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashiuya, Hussein Akilimali, Pius , Ibrahim Ajib na Tambwe.
Wachezaji wanne watajiunga na timu baadaye kambini Morogoro, ambao ni kipa Beno Kakolany, beki Hassan Kessy na Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji Donald Ngoma.
No comments:
Post a Comment