tuwasiliane

Saturday, July 29, 2017

Kocha wa The Uganda Cranes ang'atuka

Milutin 'Micho' Sredojevic amesitisha kandarasi yake na timu ya taifa ya soka nchini Uganda The Cranes akilalamikia kutolipwa mshahara.
Milutin 'Micho' Sredojevic amesitisha kandarasi yake na timu ya taifa ya soka nchini Uganda The Cranes akilalamikia kutolipwa mshahara.
Hatma yake kama kocha wa Cranes ilizungukwa na uvumi wiki yote ambao ulimfanya kukutana na maafisa shirikisho la soka Uganda FA siku ya Jumatatu.
Siku ya Jumamosi Micho alithibitisha kwa BBC Sport kwamba anawacha wadhfa wake.
''Ni notisi ya kusitisha huduma zangu kwasababu ya kutolipwa mshahara'' , alisema raia huyo wa Serbia.
''Imezidi sasa siwezi kurudi''.
Micho amekuwa mnkufunzi wa Uganda Cranes tangu alipoajiriwa mnamo mwezi Mei 2013.
Wakati wa kipindi chake kama mkufunzi wa Cranes, aliiongoza timu hiyo kufika katika fainali za kombe la mataifa bingwa Afrika Chan nchini Gabon baada ya kipindi cha miaka 39 bila kufuzu.
Hatahivyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita amekumbwa na utata unaozunguka mshahara wake na amekiri katika mitandao ya kijamii kwamba amekuwa akipata maombi mengine.
Sasa anasema kuwa swala la mishahara limechukua muda mrefu kusuluhishwa.
Micho ana historia na soka ya Afrika baada ya kuifunza Ethiopia, Sudan, Afrika Kusini, Tanzania na Rwanda.

No comments:

Post a Comment