Azam FC wamemsainisha mkataba wa miaka mitatu golikipa wa timu ya taifa ya Ghana kwa wachezaji wa ndani(CHAN), Razak Abalora.
Nyanda huyo kutoka klabu ya WAFA SC ya nchini humo, anahamia Azam FC akiwa na rekodi ya kutoruhusu bao hata moja kwenye mechi 12 za ligi kuu kati 22 alizocheza msimu huu.
Kuondoka kwake kunamfanya kocha wa timu ya taifa, Kwesi Appiah, aumize kichwa kutafuta mbadala wake kati Felix Anan wa klabu ya Asante Kotoko aliyekuwa kipa namba mbili nyuma ya Razak au Richard Ofori wa klabu ya Wa All Stars aliyekuwa namba tatu au amuite Joseph Addo wa klabu ya Aduana Stars ambaye amekuwa akumuita na kumuacha. Timu ya taifa ya Ghana kwa wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) inajiandaa na mchezo dhidi ya Burkina Faso mwezi ujao.
KLABU YAKE
Anatokea klabu ya WAFA SC (West African Football Academy Sporting Club) inayomilikiwa na klabu ya Feyenoord Rotterdam ya Uholanzi.
Ilianzishwa 1998 kama akademi ya Feyenoord kwa ajili ya kuendeleza vipaji vitakavyokuja kuitumikia hapo baadaye. Mchezaji wa kwanza kupatikana alikuwa Mohammed Abubakari aliyekwenda Uholanzi 2004.
Akademi hiyo ikajikuta inakuwa na kuanzisha timu itakayoshiriki ligi. Timu hiyo ilianza kwa jina la Feyenoord Academy na mwaka 2004 ilikapanda daraja mpaka ligi kuu na kudumu kwa misimu minne kabla ya kushuka 2007. Mwaka 2016 wakarejea tena ligi wakiitwa WAFA SC. Hii ni akademi kubwa kuliko zote Afrika Magharibi.
LIGI YA GHANA BHANA
1. Haina Mvuto
-Licha ya kuibua vipaji vikubwa vinavyotamba duniani, ghana ni moja ya nchi ambazo ligi zake hazina mvuto kabisa. Ni timu mbili tu, zile kubwa na kongwe, za Hearts of Oak na Asante Kotoko ndizo zenye uwezo wa kuvutia watazamaji angalau 10,000 kwenye mechi zao.
2. Kama wanaigana majina
-Kuna timu inaitwa Hearts of Oak(Nyoyo za mikoko) na kuna timu inaitwa Hearts of Lions(Nyoyo za Simba)
-Kuna timu inaitwa Berekum Chelsea(timu ya zamani ya babu Hans) na pia kuna timu inaitwa Berekum Arsenal (japo ilishuka 2013).
No comments:
Post a Comment