tuwasiliane

Saturday, January 7, 2017

NGOMA,AJIBU,BUSUNGU,KAMUSOKO KUPATIKANA BURE MWISHO WA MSIMU HUU WA VPL

Malimi Busungu
Ligi Kuu Bara ipo kwenye mapumziko ya muda mfupi kupisha mashindano ya Mapinduzi ambalo lina jumuisha klabu kutoka bara za SimbaAzam na Yanga, mashindano hayo yanayo tarajiwa kudumu kwa wiki mbili yalianza mwishoni mwa mwaka jana na yanatarajiwa kukamilika tarehe 12 Januari 2017

Ligi imesimama kwa muda na msimamo kwa asilimia kubwa umeendelea kubakia vile vile, Simba bado  anaongoza kwa tofauti ya alama 4, akifatiwa na Yanga, huku Azam na Mtibwa wakikamata nafasi ya tatu na ya nne kwenye msimamo

Ukiachana na klabu kupambana kwenye Ligi , pia timu zimekuwa zikipambana kuhakikisha nyota wake wanapata mikataba mipya kabla ile ya awali kufika kikokomo , klabu  hufanya hivyo angalau hata mchezaji akiamua kuamia upande wa pili nao wafaidike kidogo kuliko kwenda bure
klabu zote 16 zinatarajiwa kuhasirika kwa kuondokewa na mastaa wao bure bila wao kufaidika na chochote, kutokana na mifumo mbovu ya kimikataba ndiyo chanzo kinacho fanya timu zetu kukosa pesa pindi mchezaji akiamua kuondoka

HEAVYTALIO.BLOGSPOT.COM inakuletea orodha ya wachezaji nyota ambao mikataba yao inamalizika mwezi wa sita mwaka huu na watapatikana kwa uhamisho huru

Jonas Mkude
Tayari amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya Msimbazi, kiungo huyu amebakiza miezi 5 kwenye mkataba wake wa kuitumikia Simba, kufikia mwezi wa sita kiungo huyu atakuwa huru kwenda sehemu yeyote bila wasi wasi huku Mnyama akikosa pesa ya uhamisho kama akipata timu nyingine

Malim Busungu
Straika wa zamani wa Mgambo JKT, Busungu amepoteza jina ndani ya kikosi cha Yanga tofauti na mwaka mmoja nyuma, mshambuliaji huyo anaye sugua benchi anatazamiwa kumalizana na Wana Jangwani baada ya mwisho wa msimu huu unaotarajiwa kufika tamati mwezi wa sita na kuwa mchezaji huru

Ibrahim Ajibu
Kama ilivyo kwa Mkude pia naye Ajibu amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya Msimbazi huku akisubiri mkataba wake unao isha miezi 4 mbele, kuna dalili kubwa ya ajibu kupata ofa nono kutoka klabu za nje maana amekuwa huko akifanya majaribio kwenye vipindi tofauti tofauti

Donald Ngoma
Ali saini mkataba wa miaka miwili ndani ya Yanga, mkataba unaotarajiwa kumalizika baada ya msimu huu, Mzimbabwe huo amekuwa na mchango mkubwa kikosini kuna uwezekano wa kuondoka bure kama Yanga wasipo kuwa makini kwenye hili

Awadhi Juma
Ana kipiga na Mwadui kwa mkopo akitokea Simba, Awadhi Juma naye amebakiza miezi michache ili kumalizana na Mnyama ili hawe huru mwishoni mwa msimu, kiungo huyu maarufu kama Mandieta ni mmoja wa nyota watakao ondoka Simba bila klabu kuambulia chochote

No comments:

Post a Comment