tuwasiliane

Tuesday, January 10, 2017

Manchester United kuikabili Wigan Athletic raundi ya nne FA

Manchester United kuikabili Wigan Athletic raundi ya nne FA
Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Manchester United wamepangwa kucheza dhidi ya Wigan Athletic katika uwanja wa Old Trafford mechi ya raundi ya nne michuano ya mwaka huu.
Miamba hao waliishangaza Manchester City miaka minne iliyopita katika fainali hizo Ben Watson alipofunga dakika za majeruhi kuiwezesha timu yake kushinda 1-0 dhidi ya timu iliyokuwa ikinolewa na Roberto Mancini.
Droo hiyo iliyofanyika Jumatatu usiku, pia iliipanga Leicester City kukutana na Derby County ambao walitwaa ubingwa wa Kombe la FA 1946.
Chelsea na Tottenham Hotspur zote zitakuwa nyumbani dhidi ya timu za ligi ya chini Brentford na Wycombe Wanderers mtawalia.
Plymouth Argyle watacheza nyumbani dhidi ya Wolverhampton Wanderers iwapo wataifunga Liverpool katika mechi yao ya marudiano, wakati Arsenal wakitarajiwa kumkabili mshindi baina ya Southampton na Norwich City na Manchester City wataikabili Crystal Palace au Bolton Wanderers.
Thawabu ya Millwall kuifunga Bournemouth ni kuikaribisha timu nyingine ya Ligi Kuu Watford, wakati Sutton United ikiwa timu changa zaidi kwenye michuano itaikabili Cambridge United au Leeds United iwapo watashinda mechi ya marudiano dhidi ya AFC Wimbledon.
Raundi ya nne inawakilisha hatua ya timu 32 za mwisho kwenye michuano, na mechi zote zimepangwa kupigwa kati ya Januari 27 na Januari 30.
Droo kamili:
Tottenham Hotspur vs. Wycombe Wanderers
Derby County vs. Leicester City
Oxford United vs. Newcastle United or Birmingham City
AFC Wimbledon or Sutton United vs. Cambridge United or Leeds United
Plymouth Argyle or Liverpool vs. Wolverhampton Wanderers
Southampton or Norwich City vs. Arsenal
Lincoln City or Ipswich Town vs. Brighton & Hove Albion
Chelsea vs. Brentford
Manchester United vs. Wigan Athletic
Millwall vs. Watford
Rochdale vs. Huddersfield Town
Burnley or Sunderland vs. Fleetwood Town or Bristol City
Blackburn Rovers vs. Barnsley or Blackpool
Fulham vs. Hull City
Middlesbrough vs. Accrington Stanley
Crystal Palace or Bolton vs. Manchester City

No comments:

Post a Comment