Diego Costa Chelsea 04012017
Diego Costa amechanganywa na ofa nono kutoka China na habari zinadai kuwa huenda akaondoka Chelsea kabla ya dirisha la uhamisho Januari kufungwa
Mustakabali wa Diego Costa kwenye klabu ya Chelsea umekuwa na maswali mengi baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Hispania kuchanganywa na ofa nono kutoka Ligi ya China.
Costa, 28, alihusishwa vikali na tetesi za kutaka kuondoka Chelsea majira ya joto, lakini hatimaye alibakia London na amefunga mabao 14 Ligi Kuu Uingereza kuipeleka Chelsea kileleni mwa msimamo wa ligi msimu huu.
Hata hivyo, kwa muhibu wa habari zilizo nyingi, ofa kutoka China huenda zikamfanya Costa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, zimemchanganya mchezaji huyo hadi kukosa utulivu na kuweka mustakabali wake mashakani.
Telegraph kimeripoti kuwa Mzaliwa huyo wa Brazili huenda asicheze mechi ya Chelsea wikiendi hii dhidi ya Leicester City kufuatia kupishana na kocha Antonio Conte.
Inafahamika kuwa Costa hajafanya mazoezi na kikosi cha Chelsea zaidi ya siku tatu zilizopita, hivyo kuchochea tetesi kuwa huenda akaondoka kwenye Asia katika dirisha la uhamisho la Januari.