tuwasiliane

Friday, January 6, 2017

AJIB AGOMA KUONGEZA MKATABA NA SIMBA SC

Azam vs Simba - Ibrahim Ajibu
Mshambuliaji wa klabu ya Simba  Ibrahim Ajibu,  amegoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na kuutaka uongozi wa timu hiyo kusubiri hadi  mwishoni wa msimu  ambapo tayari klabu tatu zimeonyesha nia ya kumsajili kama mchezaji huru .

Ajib ameiambia Goal, hataki kuwa na haraka kwa sasa anachotaka ni kufanya maamuzi sahihi ambayo hayatamfanya ajutie na muda mzuri kwake ni baada ya msimu kumalizika ndiyo atakuwa huru kufanya maamuzi yake ikiwemo kuwashirikisha watu wa karibu.

“Nafurahi kuona uongozi pamoja na benchi la ufundi wametambua mchango wangu kwenye timu ndiyo maana wanataka kuniongeza mkataba lakini kwasasa ni mapema sana tusubiri kwanza ligi iishe na baada ya hapo tutakaa na kuaza mazungumzo ya mkataba mpya,”amesema Ajibu.
Katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemela, amesema hofu yao ni kumpoteza bure mchezaji huyo kutokana na kuwepo na fununu kwa baadhi ya timu kutoka nje ya Tanzania kumuhitaji ili aweze kujiunga nazo.

Kahemela amesema wamejitahidi sana lakini zoezi hilo limekuwa gumu na imebidi wasubiri kwanza michuano ya Kombe la Mapinduzi ipite ndipo waweze kuendelea kumshawishi labada anaweza kukubaliana.
“Zoezi limekuwa gumu na hofu yetu kama viongozi ni kumpoteza bure Ajibu, kwasababu ni mvhezaji ambaye tumemmlea wenye tangu mdogo hadi hapo alipofika sasa endapo tutakaa naye hadi msimu kwisha anaweza kuondoka na sisi tusifaidike na chochote kutoka kwetu,”amesema Kahemela.

Hivi karibuni mchezaji huyo alikuwa nchini Misri kwa majaribio kwenye klabu ya Haras El Hodoud, na majaribio yalisema amefaulu na kufanyiwa vipimo vya afya lakini chakushangaza mchezaji huyo alirudi nyumbani baada ya timu hiyo kuchelewa kukamilisha taratibu za usajili hivyo hofu ya Simba nikwamba huenda timu hiyo inasubiri mchezaji huyo amalize mkataba wake ili imchukue akiwa mchezaji huru.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga nao walikaribia kumsajili Ajibu kwenye dirisha dogo mwezi Desemba, lakini mpango huo ukayeyuka, ingawa bado inasemekana Yanga wana akili kama za Hodoud, wanaotaka mchezaji huyo kumaliza mkataba wake ili wamchukue free.

No comments:

Post a Comment