tuwasiliane

Friday, December 9, 2016

Tetesi hai;Lwandamina kumtoa Chirwa kwa Mkopo

Lwandamina kumtoa Chirwa kwa Mkopo?
Kocha wa Yanga Mzambia George Lwandamina , amesema na pamoja watu kuona kikosi chake kimekamika, lakini kwa upande wake anaona bado timu hiyo inamapungufu makubwa kutokana na ugumu wa michuano ya kimataifa inayowakabili mapema mwakani.
Lwandamina ambaye ana wiki ya pili tangu alipothibitishwa na uongozi kuwa kocha wa Yanga, akichukua mikoba ya Mdachi Hans Pluijm, amekiambia chanzo chetu , timu yake inahitaji mchezaji mwingine mmoja mwenye uzoefu na mashindano ya kimatafa ili iweze kufika kule inapokusudia.
“Nakubali uwezo na ubora wa wachezaji niliowakuta Yanga, hata rekodi yao ya msimu uliopita hadi walipofika inajieleza lakini, malengo ya msimu huu ni tofauti tunataka ubingwa wa Afrika hivyo lazima tuwe na timu madhubuti ambayo itaweza kupambana na timu yoyote kubwa na kupata matokeo, tayari tumempata Justine Zulu, itapendeza kama tutapata mshambuliaji mmoja  mwenye uzoefu na michuano hiyo ili timu kuweka uwiano,” amesema Lwandamina.

Kocha huyo ambaye msimu uliopita aliifikisha Zesco United , hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, amesema hana shaka na uwezo wa washambuliaji waliopo Donald Ngoma na Amissi Tambwe , lakini angependa kuwaongezea mtu mwingine ambaye atakuwa na utofauti kidogo na wao ili kuongeza changamoto ya kupigania namba ya kuanza kikosi cha kwanza.
Amesema sababu ya kutaka kuleta mshambuliaji mwingine ni baada ya kugundua kuwa timu hiyo imekuwa bingwa wa kutengeneza nafasi lakini washambuliaji wake wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi kitu ambacho siyo kizuri kwenye mchezo wa soka hasa michuano hiyo ambayo inawakabili mbele yao.
“Nimeona Yanga ndiyo inaongoza kwa kufunga mabao mengi katika ligi ya misimu mitatu iliyopita, lakini hata ukiangalia rekodi hiyo katika mchezo mmoja mmoja ni nzuri inaridhishwa kwa kweli lakini ubaya wao wanaweza kufunga mabao matatu wakapoteza nafasi saba hadi nane tena za wazi ndiyo maana nataka kuleta mtu ili kurudisha umakini wa hawa waliopo,” amesema Lwandamina.
Zipo taarifa ambazo zinadai kocha huyo ana mpango wa kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Obrey Chirwa ili nafasi yake kumleta mshambuliaji wa AC Léopards  ya Congo Brazzavile Winston Kalengo ili kuwaongezea nguvu Ngoma na Tambwe katika mashindano mbali mbali  ambayo timu hiyo itashiriki.
Yanga itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mapema mwakani baada ya kutwaa ubingwa wa Tanzani Bara, msimu uliopita na kupata nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment