tuwasiliane

Saturday, December 31, 2016

Serena Williams achumbiwa

Serena
Nyota wa mchezo wa mpira wa tennis, Serena Williams, ameweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mmoja wa waanzilishi wake Alex Ohanian kwenye mtandao wa kijamii.
Katika shairi aliloliweka katika ukurasa wake aliandika jinsi Alex alivyompeleka katika mgahawa mmoja mjini Rome, eneo ambalo walikutana kwa mara ya kwanza mwaka mmoja uliopita.
Siku ambayo alipiga magoti na kuweka pete kwenye kidole chake na kusema maneno manne na yeye akasema ndio.
Mwezi wa saba, Willliams alishinda medali ya Wimbledon kwa mara ya saba na mwezi wa tisa aliweza kuchukua nafasi ya Roger Federer', ambaye alikuwa mshindi wa mechi za Grand MATCH kwa kipindi kirefu

No comments:

Post a Comment