tuwasiliane

Sunday, December 18, 2016

Real Madrid yashinda kombe la klabu bingwa duniani

Ronaldo na Benzema wakishereherekea ushindi wa klabu yao
Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick na kuinusuru Real Madrid kuishinda klabu ya Japan Kashima Antlers katika muda wa ziada ili kushinda taji la klabu bingwa duniani.
Real ilichukua uongoza kunako dakika ya tisa kupitia mshambuliaji Karim Benzema, lakini Gaku Shibasaki alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili ili kuiweka mbele Kashima.
Ronaldo hatahivyo alisawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya Lucas Vazquez kuchezewa visivyo na Shuto Yamamoto.Mshindi huyo wa tuzo la Ballon d'Or baadaye aliiweka kifua mbele timu yake baada ya kupigiwa pasi nzuri na Benzema, kabla ya kukamilisha hat-trick yake dakika saba baadaye.
Ushindi huo unaipatia Real Madrid kombe la pili la klabu bingwa dunia na kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa katika mechi zote hadi mechi 37.
Hatua hiyo ina maana kwamba washindi 10 wa taji hilo wanatoka bara Ulaya.

No comments:

Post a Comment