tuwasiliane

Friday, December 23, 2016

Migi ameibukia Kenya

img-20161222-wa0055
Kiungo aliyetemwa na klabu ya Azam FC na APR mnyarwanda Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Gor Mahia ya Kenya inayoshiriki Kenyan Premier League (KPL) kwa lengo la kukamilisha usajili.
Taarifa zinadai kuwa, huenda muda wowote Migi akatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Gor Mahia na kuungana na nyota wengine wa kigeni katika kikosi hicho kama Medy Kagere, Godfrey Walusimbi na wengine.
Migi aliachwa na Azam FC katika kipindi cha dirisha dogo la usajili wa ligi kuu Tanzania bara ambalo limefungwa hivi karibuni.
Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd aliwahi kusema kuwa, Azam imeachana na mchezaji huyo na anaelekea nchini Vietnam kucheza soka la kulipwa.
Migi alikuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia Azam kutwaa taji la Kagame Cup kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo huku wakiweka rekodi ya kutoruhusu goli katika muda wa kawaida wa mechi zote.
Wakati huohuo, Denis Kitambi aliyekuwa kocha msaidizi wa Azam FC katika kipindi cha Stewart Hall anafanya mazungumzo na klabu ya FC Leopards ya Kenya kwa ajili ya kumsaidia Hall.
Kitambi atachukua nafasi ya Ezekiel Akwana na Nicholas Muyoti ambao walifukuzwa mwishoni mwa mwezi wa October.

No comments:

Post a Comment