tuwasiliane

Saturday, December 31, 2016

Manara aipa sifa tele Simba na kuidhihaki Yanga

Hajji Manara msemaji wa Simba

Msemaji wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi  Haji Sunday Manara amewakashifu watani wao wa jadi  klabu ya Yanga kwa kitendo chao cha kutowalipa mishahara na posho  wachezaji wake hivyo kuishi kwa kutanga tanga tanga tu
Kupitia akaunti yake ya instagram Haji Manara amewapiga kijembe Wana Jangwani kwa kitendo chao cha kujiita wa kimataifa wakati ili hali wana shindwa kuwalipa wachezaji mishahara na posho zao kwa wakati 
Haji Sunday  Manara  ameandika " Timu inayojiita ya kimataifa wachezaji wake hawajalipwa mishahara mpaka sasa wanaish kwa vifurushi vya siku huku wakilia njaa"
Hali kadhalika msemaji huyo wa Msimbazi  Haji Manara amezungumzia bahati waliyo kuwa nayo klabu ya Simba kuwa ndiyo timu pekee duniani kushabikiwa na Raisi wa nchi pamoja na Waziri Mkuu wake katika awamu mmoja ya uongozi Serikalini  ".Tanzaniani nchi pekee ambayo ina Rais na Waziri Mkuu wote mashabiki wa Simba"
Kwa muda mrefu Yanga kupitia msemaji wao aliye fungiwa na TFF Jerry Muro,  wamekuwa wakiwatania wapinzani wao klabu ya Simba kwa kuwaita wa mchangani huku wao wakiji nasibu ni kimataifa,  hasa kutokana na ushiriki wao wa mara kwa mara kwenye  michuano ya kimataifa kama klabu bingwa Afrika au Shirikisho.

No comments:

Post a Comment