Kaburu wa Simba
Makamu wa rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange 'Kaburu',  amesema timu yao ipo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wazawa, kabla ya pazia la dirisha dogo kufungwa Desemba 15.
Kaburu ameKiambia CHANZO CHETU, kikosi chao kimedhamiria kutwaa ubingwa msimu huu na ndiyo maana wamekuwa wakiweka nguvu kubwa kuiandaa timu yao ili kuweza kutimiza hilo.
“Tunataka ubingwa hakuna kingine ndiyo maana tumemsajili kipa Daniel Agyei, na tunaye kiungo James Kotei, ambaye anafanya majaribio kama mambo yakienda sawa tutamsajili pia tunatarajia kuwatambulisha wachezaji wapya wawili wazalendo ambao tutawasajili kabla ya dirsha kufungwa,”amesema Kaburu.
Kiongozi huyo amesema kocha wao aliawaagiza kuongeza mshambuliaji mmoja na beki wa kati mmoja na hadi sasa mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote wiki hii wanatarajia kuwatangaza, baada ya kumalizana nao.
Kaburu amesema kwasasa bado wapo kwenye mazungumzo na timu zinazo wamiliki wachezaji hao ndiyo maana wamefanya ukimwa mkubwa, lakini baada ya kumalizana na timu wanazozichezea watawatambulisha kwa mashabiki wao,”amesema Kaburu.
Kiongozi huyo pia amezungumzia taarifa za kumsajili beki Mbuyu Twite, na kudai hawana mpango ya kumsajili mchezaji huyo kwasababu ripoti ya kocha wao haijaonyesha kumchukua mchezaji wa aina yake.
Amesema Simba ni timu ambayo inaundwa na wachezaji wengi vijana hivyo kwa umri wa Mbuyu Twite itakuwa ni vigumu kutokana na mipango waliyokuwa nayo ya kucheza michuano ya kimataifa mwakani ambapo mchezahi huyo hatoweza kuhimili mikikimikiki kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
Kaburu amesema timu yao itandelea kubaki Kambini Morogoro, na itakuwa huko hadi zikiwa zimebaki siku tatu ambapo watarejea Dar es Salaam kuelekea Mtwara ambapo wataanza mechi yao ya mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda FC.