tuwasiliane

Friday, November 11, 2016

Wenger aiomba Chile 'isimchezeshe' Sanchez

Alexis Sanchez
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameiomba Chile kutomuweka hatarini mshambuliaji Alexis Sanchez mechi ya taifa hilo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay.
Sanchez, 27 ,alikosa mechi ambayo Chile walitoka sare 0-0 naColombia Alhamsii baada yake kupata jeraha la misuli.
Matabibu wa Chile wamekuwa wakitumai atapata nafuu kwa wakati kuweza kucheza mechi hiyo dhidi ya Uruguay Jumanne mjini Santiago.
"Huwa anapenda kucheza na kila wakati huwa tayari kucheza hata anapoumia," Wenger aliambia beIn Sports.
Sanchez, amefunga mabao manane mashindano yote msimu huu akichezea Arsenal.
Hakucheza miezi miwili msimu uliopita baada ya kuumia misuli ya paja.
"Ni kizungumkuti na lazima tulinde afya ya Alexis Sanchez," Wenger amesema.
"Lazima matabibu wetu waweze kuangalia uchunguzi wa MRI na kuona uzito wa jeraha na kuwa na uhakika kabisa kwamba uamuzi kuhusu kuchezeshwa kwake hautamwathiri siku za usoni."

No comments:

Post a Comment