Wachezaji watano nyota Afrika ambao watapigania tuzo ya BBC inayotolewa kwa Mwanakandanda Bora Afrika wa mwaka watatangazwa Jumamosi na upigaji kura kuanza.
Majina ya wachezaji hao watakaoshindania tuzo ya mwaka 2016 watatangazwa kwenye kipindi cha moja kwa moja BBC World TV na kwenye redio ya BBC World Service kuanzia saa 18:00 GMT.
Mashabiki wa soka ya Afrika kote duniani watapata fursa ya kupiga kura kwenye tovuti ya BBC African football kuanzia saa 18:50.
Upigaji kura utafungwa saa 18:00 Mnamo Jumatatu, 28 Novemba na mshindi atatangazwa moja kwa moja kupitia runinga ya Focus on Africa TV na pia kwenye redio Jumatatu 12 Desemba saa 17:35.
Wachezaji nyota wa zamani Afrika pamoja na wataalamu wa soka watahudhuria kipindi hicho maalum siku ya Jumamosi.
Kipindi hicho ambacho mtangazaji wake atakuwa Peter Okwoche, kitashirikisha mahojiano na mshindi mmoja wa zamani wa tuzo hiyo, majadiliano na watakaoshindania tuzo mwaka 2016 na utathmini wa soka ya Afrika mwaka huu.
Na kutakuwa pia na fursa ya kutazama video za matukio ya nyuma ya pazia tkwenye kurasa za Facebook za BBC Africa na BBC Sport na pia kwenye Instagram.
BBC Sport pia wataandika ujumbe wa moja kwa moja kwenye Twitter uzinduzi utakapokuwa unafanyika, katika akaunti za Twitter za BBC Africa na BBC Sport.
Wanaotumia mitandao ya kijamii wanaweza kufuatilia matukio kupitia kitambulisha mada #BBCAFOTY.
Washindi wa zamani wa Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka:
2015: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast
2014: Yacine Brahimi (Porto & Algeria)
2013: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast)
2012: Chris Katongo (Henan Construction & Zambia)
2011: Andre Ayew (Marseille & Ghana)
2010: Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)
2009: Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
2008: Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Egypt)
2007: Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)
2006: Michael Essien (Chelsea & Ghana)
2005: Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)
2004: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2003: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2002: El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)
2001: Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
2000: Patrick Mboma (Parma & Cameroon)
No comments:
Post a Comment