tuwasiliane

Friday, November 11, 2016

Vijana watano wachaguliwa majaribio ya Azam FC U-17 Zanzibar

KAMA ulimisi taarifa ya majaribio ya wazi ya mwisho ya Azam FC kwenye msako wa kusaka vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) yaliyofanyika Visiwani Zanzibar ndani ya Uwanja wa Amaan mwishoni mwa wiki iliyopita.
Taarifa rasmi ni kuwa tulifanikiwa kuwachagua vijana watano kutoka visiwani humo, ambao wameingia kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika mwezi ujao makao makuu wa Azam Complex, yatakayohusisha vijana wote waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali.
Vijana hao watano wanaungana na wengine 37 waliochaguliwa kwenye maeneo tofauti nchini katika mikoa ya Morogoro (12), Dar es Salaam (13), Tanga (12) na kufikisha idadi ya vijana 42 waliochaguliwa mpaka sasa kati ya vipaji 2,143 waliofanyiwa usaili.
Uongozi wa Azam FC kwa kushirikiana na idara ya ufundi ya timu hiyo, una nia dhati ya kuboresha mfumo wa kituo chake cha kukuza vipaji 'Azam FC Academy' ili kihusishe vijana wa umri tofauti kwa ajili ya kuvuna vipaji vingi zaidi kwa manufaa ya baadaye ya timu hiyo na Taifa kwa ujumla.
Hadi sasa Azam FC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye uleaji wa vipaji katika kituo hicho, ikivuna vijana kadhaa wanaotamba sehemu tofauti katika timu mbalimbali nchini, wengine wakiwa wanaing'arisha timu kubwa ya kituo hicho.
Baadhi ya waliopandishwa kwenye timu kubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Ismail Gambo, Gadiel Michael, Abdallah Kheri (mkopo Ndanda), viungo Mudathir Yahya, Masoud Abdallah, Bryson Raphael (mkopo Ndanda).
Wengine ni Joseph Kimwaga (mkopo Mwadui), Farid Mussa (aliye mbioni kujiunga na CD Tenerife - Hispania), wshambuliaji Kelvin Friday (mkopo Mtibwa Sugar) na Shaaban Idd.
Wanaotamba na timu nyingine baadhi yao ni Simon Msuva (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Rashid Mandawa (Mtibwa Sugar), Joseph Mahundi (Mbeya City), Jamal Mnyate (Simba).

No comments:

Post a Comment