tuwasiliane

Tuesday, November 8, 2016

STRAIKA LA MEDEAMA LAJA KUONGEZA NGUVU AZAM FC


MSHAMBULIAJI wa Medeama SC ya Ghana, Bernard Ofor yuko mbioni kujiunga na Azam FC ya Dar es Salaam baada ya makubaliano ya awali.
Mchezaji huyo wa zamani wa New Edubiase United ameondoka Ghana jana na anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo kumalizana washindi hao wa Ngao ya Jamii.

Akifanikiwa kusaini Azam FC, Ofori ataungana na wachezaji wengine wawili wa Medeama SC waliojiunga na Azan FC, ambao ni winga Enoch Atta Agyei na mshambuliaji Daniel Amoah.
Amoah amekwishajiunga na kikosi cha Azam FC kilicho chini ya kocha Mkuu, Mspaniola Zeben Hernandez Rodriguez wakati Agyei atajiunga na timu hiyo Januari atakapofikisha umri wa miaka 18.


No comments:

Post a Comment