tuwasiliane

Tuesday, November 29, 2016

Ngoma: aitema Yanga kutimkia Ulaya

Donald Ngoma
Mshambuliaji wakimataifa wa Yanga raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma amegoma kusaini mkataba mpya na huenda akaachana na mabingwa hao wa ligi vya Vodacom Tanzania Bara, baada ya mkutaba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Ngoma  amekiambia chanzo kimoja maarufu cha michezo kuwa,  mtazazamo wake kwa sasa ni kucheza soka Barani Ulaya, au kwenye ligi ambazo zinaushindani zaidi ya Tanzania ili kupandisha kiwango chake na kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe.

“Hii ni mikakati ambayo nimejiwekea na wala sina ubaya na mtu yeyote hapa Yanga, msimu wangu wa kwanza umekuwa na mafanikio makubwa na nimeweza kutimiza malengo ya timu kwa kubeba makombe mawili na kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ambayo ilipita miaka mingi kabla ya timu hiyo kurudia tena,” amesema Ngoma.Mshambuliaji huyo aliyeifungia Yanga mabao 24, kwenye michuano yote iliyoshiriki msimu uliopita amesema kinachomfanya kutaka kuondoka ni kutafuta changamoto nyingine baada ya kutimiza kila kitu hapa Tanzania.

Mzimbabwe huyo amesema kitendo cha kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zimbabwe ambacho kitashiriki michuano ya Mataifa ya Afrika AFCN, mapema mwakani kimemuumiza sana na amedai tatizo kubwa ni kukosekana kwa ushindani kwenye ligi ya Vodacom Tanzania.

“Siwezi kujua kama huenda nikabadili maamuzi lakini kwa sasa mpango wangu ni kubadilisha mazingira kucheza soka Ulaya najua hilo siyo tatizo kwangu kwasababu badoni nanaumri mdogo na kuna timu nyingi zimeonyesha kunihitaji,” amesema .
Ngoma  aliyewahi kutamba na FC Platinum kabla ya kutua Yanga msimu uliopita, amesema hajutii maamuzi yake ya kucheza timu hiyo ya Tanzania kwasababu amejifunza mambo mengi akiwa na vijana hao wa Jangwani lakini pia amemshukuru sana kocha Hans van der Pluijm, kwa kumuamini katika kipindi chote cha kazi.
Mkataba wa Ngoma unamalizika mwishoni mwa msimu huu na kocha mpya wa Yanga George Lwandamina ameahidi kuzungumza na kumshawishi mshambuliaji huyo ili asiondoke.

No comments:

Post a Comment