tuwasiliane

Tuesday, November 22, 2016

Mchungaji apulizia waumini Doom Afrika Kusini akidai ni tiba

Muumini akipulizwa dawa ya Doom
Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali.
Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, pmchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.
Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.
Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.
Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly katika jimbo la Limpopo, anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.

'Nguvu za Mungu'

Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa "yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".
Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha.
Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa ''nabii'' huko Limpopo - Lethebo Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:

No comments:

Post a Comment