tuwasiliane

Thursday, November 17, 2016

Mario Balotelli: "Mahusiano yangu na Brendan Rodgers Liverpool yalikuwa majanga"

Mario Balotelli: "Mahusiano yangu na Brendan Rodgers Liverpool yalikuwa majanga"
Mario Balotelli ameuelezea uhusiano wake na kocha wa zamani wa Liverpool Brendan Rodgers kama “Janga”.
Mshambuliaji huyo mtata, raia wa Itali, ambaye aliondoka Liverpool majira ya joto kujiunga na Nice ya Ufaransa, amemtaja Brendan Rodgers kuwa miongoni mwa makocha asiokuwa na mapenzi nao.
Balotelli alishangaa kununuliwa na Rodgers alipojiunga na Reds akitokea AC Milan miaka miwili iliyopita kwa dau la paundi milioni 16, lakini alishindwa kumshawishi kocha huyo, akifunga goli moja tu Ligi ya Uingereza katika msimu wa 2014-15.Baada ya mshambuliaji huyo kutumika kwa mkopo Milan, Jurgen Klopp ambaye alichukua nafasi ya Rodgers kama meneja wa Liverpool Oktoba mwaka jana, aliamua kumwondoa Super Mario kwa kumuuza moja kwa moja Nice, ambako amefunga magoli sita hadi sasa.
Akiwa anazungumzia mameneja wake wa zamani, nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alikiri kuwa Roberto Mancini alikuwa kocha wake kipenzi, aliyefurahia kucheza kwenye kikosi chake akiwa Inter Milan na klabu ya Manchester City, huku Brendan Rodgers akiwa mkiani kabisa mwa orodha hiyo.
“Kwangu mimi, bado Mancini ndiye bora kuliko wote; mtu safi sana, nina deni kubwa sana kwake,” Balotelli aliliambia Gazzetta dello Sport. “Nafasi ya pili nampatia [Lucien] Favre [wa Nice] pamoja na [Jose] Mourinho; Mreno huyu ana kipaji kikubwa sana na hamasa, inauma tulipishana kidogo.
“Mbovu kuliko? Si Klopp, na wala sina jazba naye. Kama kuna hali aliifanya akiwa Liverpool, huenda angenivumilia zaidi. Kwa kweli, nilivunjika moyo sana kufanya kazi na Rodgers. Nilifurahia kufanya naye mazoezi lakini mahusiano yetu yalikuwa janga.”Rodgers kwa sasa ni kocha wa miamba wa Scotland Celtic.

No comments:

Post a Comment