tuwasiliane

Friday, November 11, 2016

LWANDAMINA AWASILI KIMYA KIMYA DAR TAYARI KUANZA KAZI YANGA


KOCHA mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amewasili mjini Dar es Salaam jioni ya jana tayari kusaini mkataba wa kazi na mwajiri mpya.
Lwandamina anatua nchini baada ya kumalizana na klabu yake, Zesco United ya kwao aliyoifanyia kazi tangu mwaka 2014.
Hata hivyo,  Lwandamina aishuhudia kwenye Televisheni mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho kati ya Yanga na Ruvu Shooting.
Na hiyo ni kwa sababu uongozi wa Yanga ulifikiria utamkosesha raha kocha anayemaliza muda wake, Mholanzi Hans van der Pluijm."Hatutaki kumnyima raha Babu (Pluijm).  Lwandamina alibaki tu hotelini kuangalie mechi kwenye Televisheni na baada ya hapo atapatiwa DVD za mechi nyingine zilizopita ili kuijua timu vizuri,"kimesema chanzo kutoka Yanga leo.

Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa kocha Hans van der Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

No comments:

Post a Comment