tuwasiliane

Saturday, November 26, 2016

Karelis Anavyomlaza Njaa Mbwana Samatta Genk

Mbwana Samatta of Genk & Lokomotiva's Ivan Sunjic
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta mambo yanaonekana kuwa si mazuri sana kwa upande wake kadiri siku zinavyokwenda mbele, kwa nini?
Uwepo wa Nikolaos Karelis ni kigingi kwa Samatta kupata fursa ya kuonesha uwezo kwake katika timu anayoichezea Ubelgiji KRC Genk.
Samatta anatokea benchi kwenye mechi zote alizocheza hadi sasa kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa ugiriki Karelis Nikolous. Lakini katika mechi waliyoshinda 1-0 dhidi ya Genk Samatta alipewa muda mchache zaidi wa kucheza akiingia dakika ya 85 kuchukua nafasi ya Karelis, dakika chache hizo zilizobaki hazikumtosha Mtanzania huyo kufanya madhara yoyote.
Ushindi wa bao 1-0 iliopata KRC Genk dhidi ya Rapid Wien unaipa nafasi timu hiyo inayotumikiwa na Mbwana Samatta kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano ya Ligi ya Uropa msimu huu.Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji raia wa Ugiriki Nikolaos Karelis dakika ya kumi na moja tangu mchezo kuanza.
Nahodha wa timu ya taifa ya Taifa Stars Mbwana Samatta, aliingia uwanjani dakika ya 85 akitokea benchi kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao Nikolaos Karelis.
Matokeo hayo yanaifanya KRC Genk kufikisha jumla ya pointi 9 baada kucheza mechi 5 za Kundi F na kuongoza kundi hilo kwa tofauti ya magoli mbele ya Athletic Bilbao ambao wanalingana kwa idadi ya pointi na mechi walizocheza.
Genk inasubiri kucheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi itakayoamua timu ipi itaongoza Kundi F wakati Sassuolo na Rapid Wien zenyewe zikisubiri kukamilisha ratiba kwa sababu tayari zimeshatupwa nje ya mashindano hayo.
Je! Mbwana Samatta atapata nafasi japo kuanza kwenye mechi hiyo ya mwisho?

No comments:

Post a Comment