tuwasiliane

Friday, November 11, 2016

Argentina hoi kwa Brazil yachapwa 3-0

Brazil
Michezo mitano ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mwaka 2018, imecheza kwa ukanda wa Marekani Kusini.
Brazil wakicheza katika dimba la Belo Horizonte, wamewachapa Argentina kwa mabao 3-0, mabao ya brazili yakifungwa na Philipe Couthino, Neymer, na Paulinho.
Venezuela wakicheza nyumbani nao wameibuka na ushindi wa kishindo kwa kuwachapa bolivia kwa mabao 5-0.


Paraguay wamekubali kichapo nyumbani baada ya kufungwa mabao 4-1 na Peru,Uruguay wakashinda kwa mabao 2 - 1 dhidi ya EcuadorColombia wakashindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoshana nguvu na Chile kwa sare ya bila kufungana.

No comments:

Post a Comment