tuwasiliane

Thursday, February 11, 2016

SERENGETI BOYS KUANZA NA SHELISHELI

Shirikisho la mpira wa miguu barani afrika (caf) limetoa ratiba ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.
Michuano hii itakazofanyika nchini madagascar mwakani huku timu ya taifa ya tanzania itaanza mchezo wake dhidi ya shelisheli
Katika ratiba hiyo iliyotolewa makao makuu ya caf, cairo misri na nakala yake kutumwa kwa tff, tanzania imepangwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya shelisheli kati ya juni 24,25,26 nchini na marudaino kuchezwa julai 01,02,03 nchini shelisheli.
Mshindi kati ya mchezo huo namba 15 na16 atacheza dhdi ya timu ya taifa ya afrika kusini katika hatua inayofuata ya 16 bora, na kisha baadae kupata timu 8 zitakazofuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini madagascar mwakani.

No comments:

Post a Comment