tuwasiliane

Wednesday, January 27, 2016

YANGA KUTIMKIA AFRIKA YA KUSINI KUJIANDAA NA KLAB BINGWA AFRIKA

Yanga-pipa
YANGA imevunja ratiba yao ya kucheza na Coasta Union katika mchezo wa Ligi baada ya kutangaza kikosi chao kwenda Afrika Kusini katika mashindano mafupi.
Mkuu wa Idara na Mawasiliano ya Yanga Jerry Muro amesema kikosi chao kinatarajiwa kuondoka nchini Ijumaa ya wiki hii tayari kwa mashindano hayo ambayo hata hivyo hawakuyaweka wazi.
Muro amesema safari hiyo inataka kutumiwa na kikosi chao katika kujiweka sawa kabla ya kuanza mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo timu hiyo itafungua dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius kati ya Februari 12-14.
“Barua rasmi itapelekwa TFF na Katibu wetu Baraka Deusdedit kesho kuweza kuwajulisha kwamba tunalazimika kwenda huko baada ya uongozi wetu kukubali mualiko huo ambao ulifika muda tu lakini kuna mambo tulitaka yawekwe sawa,” amesema Muro.
“Kwasasa timu tutakazocheza nazo tutaziweka wazi baada ya kupata ratiba lakini pia ikumbukwe kwamba tunashiriki Ligi ya Mabingwa sasa tutatumia nafasi hiyo kama sehemu ya maandalizi.”

No comments:

Post a Comment