tuwasiliane

Friday, January 8, 2016

Samatta,jogoo wa Afrika





Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.Huku tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borusia Dotmund nchini Ujerumani.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.
Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon
Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Cote d’IvoreKocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo.
Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo
Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon
Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini Gambia
Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

No comments:

Post a Comment