Kenya Paul Kiongera in action for Simba of Tanzania.
Mshambuliaji wakimataifa wa Simba raia wa Kenya Paul Kiongera amesema kocha Jackson Mayanja amezidi kumweka katika wakati mgumu kutokana na kutompa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Kiongera amekiambia chanzo kimoja, kiwango chake kimekuwa kikishuka kwa kasi na hiyo inatokana na kukaa benchi kwa muda mrefu bila kujua sababu za msingi kutoka kwa Mganda huyo ambaye amepewa timu wiki mbili zilizopita baada ya kutimuliwa kwa kocha Muingereza Dylan Kerr.
“Najua kunaushindani mkubwa kwenye kikosi cha Simba lakini kiwango nilichokuwa nacho naamini ninaweza kupata nafasi japo siwezi kumlazimisha kocha kwasababu yeye ndiye mwenye kujua mtu sahihi wa kumtumia katika mipango yake,”amesema Kiongera.
Kiongera amerejea Simba kwenye dirisha dogo akitokea KCB, timu aliyokuwa akiichezea baada ya kupona majeruhi yaliyosababisha atolewe kwa mkopo kwenye timu hiyo ya zamani.