Mambo ya dirisha dogo la usajili yamepamba moto, Kila timu inakazana kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu Bara.
Yanga leo inatarajia kumpokea mshambuliaji wa kimataifa kutoka Niger, Issoufou Boubacar Garba ambaye anakuja kufanya majaribio kabla ya kusajiliwa endapo atapewa kiwango chake kitamvutia kocha Hans van der Pluijm.
Garba wa Yanga
Pluijm amekiambia chanzo chetul, kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya kuachana na kiungo Mbrazili Andrey Coutinho, na ameamua kumleta Garba, ili kuweza kuendana na muda kabla ya dirisha halijafungwa.
“Nimshambuliaji hodari mwenye uwezo mkubwa kutokana na klabu alizopitia Tunisia na kwao Niger anapocheza kwa sasa naamini kama atafanikiwa atakuwa na mchango mkubwa kwa Yanga kwani nimekuwa nikimfuatilia kwa kwa karibu anafaa kuwa na sisi,”amesema Pluijm.
 Pluijm amepewa nafasi hiy baada ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji, kukataa timu hiyo kusajili wachezaji kutoka nchi jirani za Uganda na Kenya kutokana na usumbufu wa mara kwa mara waliokuwa nao.
Garba kwa sasa anaichezea klabu ya AS Douanes, ambayo ndio mabingwa wa Niger na hiyo ni baada ya kuachana na timu za Club Africain,ES Hammam- Sousse ya Tunisia.