tuwasiliane

Friday, December 18, 2015

Guardiola kuweka wazi hatima

Pep
Mkufunzi mkuu wa Bayern Munich Pep Guardiola anasema kuwa ataelezea "wazi" kuhusiana na mustakabali wake ligi ya Bundesliga juma lijalo.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 44, ambaye amehusishwa na klabu ya timu ya Manchester City, ameiongoza Bayern kunyakua mataji mawili tangu achukue hatamu za ukufunzi mwaka 2013, lakini mkataba wake unafikia kikomo mwezi Juni.
Gazeti moja la Uhispania la Marca, limeripoti jana Jumatano kuwa Guardiola tayari ameiambia Bayern kuwa ataondoka klabu hiyo.
Gazeti hilo la Madrid linadai kuwa liaamini kuwa pande zote mbili, yeye pamoja na klabu, zitafaidika na mabadiliko hayo, kwa sababu bidii anayohitaji kutoka kwa wachezaji pamoja na mazoezi makali anayowafanyisha huenda yakaishia kuwaathiri.
Mwezi uliopita duru kutoka Uhispania zilidai kuwa mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona amekubali kuondoka Bayern mwisho wa msimu huu ili kuanza kuikufunza Manchester City.
Mabingwa hao wa Bavaria wamo kileleni kwa sasa ligi ya Ujerumani, alama tano mbele, wanapojiandaa kwa mechi yao ya mwisho ya mwaka 2015 ugenini Hannover Jumamosi.

No comments:

Post a Comment