tuwasiliane

Friday, August 15, 2014

CAS YAMPUNGUZIA ADHABU SUAREZ

 


Mahakama ya rufaa ya michezo imeafiki marufuku ya miezi miine aliyopewa mshambulizi wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez.
Hata hivyo Suarez amepata afueni kwani sasa ataruhusiwa kushiriki mazoezi na timu yake ya Barcelona
Wakili wa Suarez alifaulu kuishaiwishi mahakama kuwa Kauli ya FIFA ilikuwa kali kupindukia.
Shirikisho la soka duniani FIFA ilimpata na hatia Suarez kwa kumn'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipokuwa ikikabiliana na Italia katika kombe la dunia huko Brazil.

Kufuatia uamuzi huo Suarez, 27, atarejea katika mechi dhidi ya mahasimu wao Real Madrid ''El Clasico'' tarehe 26 Oktoba.
Mshambulizi huyo wa Uruguay ataendelea kutumikia marufuku ya mechi za kimataifa .

No comments:

Post a Comment