tuwasiliane

Tuesday, July 1, 2014

SUAREZ AOMBA MSAMAHA


Mshambulizi wa Uruguay na Liverpool ya Uingereza Luiz Suarez sasa amemuomba msamaha mlinzi wa Italia Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng'ata timu hizo zilipokuwa zicheza mechi ya mwisho ya makundi huko Brazil.
Suarez aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ''baada ya kuketi nyumbani na familia yangu na kutulia imenijia kuwa tukio la kumng'ata Chellini ni la kusikitisha na kwamba sitarudia tena .
“ninajutia sana tukio hilo na ninamuomba msamaha Chellini .ukweli ni kwamba anauguza jereha la kuumwa baada ya kugongana naye katika mechi hiyo .''


Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.
FIFA imeamuru asishiriki mechi yeyote ile kwa kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini ya pauni 65000. (£65,680).
Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia marufuku hiyo.

Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.



No comments:

Post a Comment