tuwasiliane

Wednesday, July 2, 2014

OFFICIAL;DIEGO COSTA ATUA CHELSEA

 Chelsea imedhibitisha kuwa imekubaliana na mshambulizi wa Atletico Madrid na Uhispania Diego Costa sasa atashuka Stamford bridge msimu ujao.
Klabu hiyo ya London imedhibitisha kuwa imeafikiana na Atletico Madrid kutumia kipengee cha kumnunua mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 25 .
Hadi kufikia sasa haijadhibitisha gharama yake itakuwa kiasi gani lakini wandani katika klabu hiyo wanasema Costa huenda akaigharimu The Blues takriban dola milioni 55m

Mzaliwa huyo wa Brazil aliifungia Atletico mabao 35 msimu uliopita na kuisadia timu hiyo kufuzu kwa fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya walikoshindwa na mahasimu wao wa jadi Real Madrid .

Kocha wa wa the Blues Jose mourinho amekuwa akiimarisha kikosi chake kwa kusajili nguvu mpya na pia kuna dukuduku kuwa wachezaji wazoefu wa Chelsea Ashley Cole na Frank Lampard huenda wakaondoka Stamford Bridge.
Mwezi uliopita Mourinho alimsajili aliyekuwa kiungo wa Arsenal Cesc Fabregas huku kandarasi ya kipa Mark Schwarzer ikiongezwa muda

No comments:

Post a Comment