tuwasiliane

Sunday, July 13, 2014

JOACHIM LOEW;ASEMA WANATWAA NDOO LEO


Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema kuwa timu yake inapania kuandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza kutoka bara Uropa kutwaa taji la dunia Kusini mwa Marekani.
Ujerumani itachuana na Argentina katika fainali ya kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil baadaye Jumapili tarehe 13 Julai katika uwanja wa kihistoria wa Maracana Ulioko mjini Rio de Jenairo Brazil.
Loew anaimani kuwa timu yake itarejesha nyumbani kombe lao la nne la dunia.


Hakuna timu yeyote kutoka barani Uropa ambayo imewahi kushindwa taji la dunia katika michuano nane ya kombe la dunia iliyoandaliwa Kusini mwa Marekani.
“Ninaamini kuwa kikosi hichi kinauwezo wa kuandikisha rekodi ya dunia fauka ya matokeo ya zamani ya timu kutoka barani Uropa''
Hii itakuwa ni mara ya Tatu kwa timu hizo kukutana katika fainali Ujerumani ikishinda mechi moja nayo Argentina ikishinda ile nyengine(1986)
Argentina ilifuzu kwa fainali hizo baada ya kuiondoa Uholanzi kupitia mikwaju ya penalti huku Ujerumani ikijikatia tikiti yake ya Fainali baada ya kuifunza soka Brazil ilipoikomoa mabao 7-1 katika ile nusu fainali nyengine.
Licha ya hayo ,Loew amemlimbikizia sifa kochokocho kocha mpinzani Alejandro Sabella akisema Argentina ameshinda mechi zao zote licha ya ushindani mkali.
Maonni yake Loew yalitiliwa pondo na kiungo wake wa kati Bastian Schweinsteiger aliyesema kuwa Ujerumani inauwezo wa kuilaza Argentina licha ya wao kuonekana wakakamavu katika safu ya ulinzi.

Kocha Loew alikanusha dhana kuwa Argentina imeumbwa kumnufaisha mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi ,''La hasha Argentina inawashambulizi wazuri hata wenye sifa sawa na Messi lakini wao ndio wanaofanya kazi ya zida kisha messi anamaliza tu .
''Huwezi kuwapuuza washambulizi kama Gonzalo Higuaín na Angel Di Maria, ukiwa unadhania Argentina ni Messi umekosea sana''alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment