tuwasiliane

Tuesday, July 1, 2014

COUTINHO AANGUKA MIAKA MIWILI YANGA
















Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil jana amesaini mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katibu mkuu wa Young Africans  Bw Beno Njovu amesema usajliwa mchezaji Coutinho ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na kama ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya.

Coutinho ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia kwenye mji wa Berem ambapo alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paysandu Sports Club kabla ya kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika klabu ya Rukhapura United.

Mpaka anajiunga na klabu ya Young Africans Andrey Coutinho alikuwa akichezea timu ya Castanhal EC iliyopo kwenye Ligi Daraja la pili ambao aliweza kuichezea kwa michezo yote  ya mzunguko wa pili mwaka 2014.

Katika hatua nyingine kikosi cha Young Africans kinatarajia kuendelea na mazoezi kesho chini ya kocha Marcio Maximo katika ufuke wa Coco Beach ikiwa ni siku yake ya kwanza na jioni katika Uwanja wa Bandari Tandika kuanza kazi baada ya leo kuwa na mkutano wa ndani na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi.
source. www, http://youngafricans.co.tz

No comments:

Post a Comment