tuwasiliane

Wednesday, July 9, 2014

BRAZIL 1 GERMAN 7 FULL TIME




Ujeruman  Ndiyo timu ya kwanza kufuzu kwenye Fainali ya kombe la dunia Brazil 2014, baada ya kuinyeshea wenyeji Brazil mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo Horizonte.

Umakini wa vijana wa Joachim Low ulikuwa wa kupigiwa mfano walipoiadhibu Brazil na kuwa timu ya kwanza kuwahi kushindwa kwa mabao mengi zaidi katika hatua hiyo ya nusu fainali ya kombe la dunia.
Kabla ya mechi hiyo vyombo vya habari vilikuwa vimemulika mfumo wake Luiz Felipe Scolari vikidai alikuwa ameumba timu yake kumtegemea Neymar.
Kujeruhiwa kwa Neymar Ijumaa iliyopita ilimlazimu Scolari kubadili mfumo ambao sasa haukuwa na nyota huyo.

Ilikuwa wazi tofauti ya mbinu za makocha hao wawili wajerumani walipoanza kwa kuwashirikisha washambulizi Miroslav Klose,Thomas Muller na Mesut Ozil huku Schweinsteigerakiwaongoza Toni Krooos Khedira na Lahm katika kiungo cha Kati.
Na Baada ya nipe nikupe ya kufungua mechi Iliwachukuwa Wajerumani takriban dakika kumi tu za kwanza kupenya safu ya ulinzi ya Brazil iliyokuwa inakosa uzoefu wa Thiago Silva
Thomas Muller alifungua kivuno hicho cha mabao kabla ya Klose kuidhibitishia Ujerumani fainali yao kombe la dunia kwa mkwaju uliomwacha kipa wa Brazil Julio Cesar asijue la Kufanya.
Klose kwa ushirikiano na Toni Kroos walifunga bao la tatu na la nne katika kipindi cha dakika moja.
Sami Kheidira alifunga la tano kunako dakika ya 29 kabla ya mchezaji wa akiba Andre Schurrle kufunga mabao ya 6 na ya 7 .
Bao la kufutia machozi la Brazil lilifungwa na Oscar kunako dakika ya mwisho ya mechi hiyo.


No comments:

Post a Comment