tuwasiliane

Thursday, July 10, 2014

ARGENTINA YATINGA FAINALI YA WORLD CUP,YAITOA UHOLANZI KWA PENATI
Argentina imejukatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.
Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia kwa mikwaju ya penalti.
Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi


Romero aliokoa mikwaju ya Ron Vlaar na Wesley Sneijder.
Wafungaji wa Argentina walikuwa ni Lionel Messi,Ezequiel Garay Sergio Aguero na kisha Maxi Rodriguez.
Argentina sasa Itachuana na Ujerumani ambayo iliweka historia kwa kuinyuka Brazil mabao 7-1katika nusu fanali.
Uholanzi ambayo sasa imeshindwa kutwaa kombe la dunia hata baada ya kufuzu kwa nusu fainali tatu mfululizo itachuana dhidi ya wenyeji Brazil siku ya jumamosi kuamua mshindi wa tatu.
Brazil ilipata kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani siku ya Jumanne.
Penalti ndizo zitakazoamua nani kati ya Uholanzi na Argentina atakutana na Ujerumani katika fainali.

No comments:

Post a Comment